Amos 9:11-15

Kurejezwa Kwa Israeli

11 a“Katika siku ile nitaisimamisha
hema ya Daudi iliyoanguka.
Nitakarabati mahali palipobomoka
na kujenga upya magofu yake,
na kuijenga kama ilivyokuwa awali,
12 bili wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu,
na mataifa yote yale yanayobeba Jina langu,”
asema Bwana ambaye atafanya mambo haya.
13 c“Siku zinakuja,” asema Bwana,

“wakati mvunaji atatanguliwa na mkulima,
naye mpanzi atatanguliwa na yeye akamuaye zabibu.
Divai mpya itadondoka kutoka milimani,
na kutiririka kutoka vilima vyote.
14 dNitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa;
wataijenga tena miji iliyoachwa magofu,
nao wataishi ndani mwake.
Watapanda mizabibu na kunywa divai yake;
watalima bustani na kula matunda yake.
15 eNitaipanda Israeli katika nchi yao wenyewe,
hawatangʼolewa tena
kutoka nchi ambayo nimewapa,”

asema Bwana Mungu wenu.
Copyright information for SwhNEN